KijijiChetu(Family)

THE KIJIJICHETU(Family)

KIJIJICHETU(Kijijifamily) ni Jina la linalotumiwa na kikundi cha hiari cha wanafamilia wa Tanzania wenye kuamini katika fikra chanya, wajibu halisia, haki na fursa katika utaifa kwa mlengo endelevu na chanya. Hili ni zao la jitihada za Wana Asasi huru ya WANAFIKIRA CHANYA WA TANZANIA -Positive Thinkers Tanzania (PTT)

KIJIJIfamily ni sehemu huru ya mijadala makini na sehemu isiyojadili kwa dhana ya kulaumu au kuegemea maeneo ya kisiasa katika ushabiki wa vyama vya siasa Tanzania. Bali ni sehemu inayoruhusu hoja, mada, uchakatuzi, uchangiaji, ujadilianaji, usuluhishaji na uhitimishaji wa masuala na changamoto za kijamii. Kwa kutumia Kijijifamily jamii itajenga taswira bora katika kutatua, kuboresha, kuanzisha,kuendeleza, kukuza, kutetea, kusaidia, kuhuisha, kuelewesha, kuonya, kufundisha, kujulisha na kutekeleza wajibu, haki na fursa katika masuala ya kijamii, kisiasa, kimazingira, kiuchumi kwa dhana chanya kwa Maslahi ya Taifa.

Kijijifamily ni chimbuko halisia katika kuziweka familia za watanzania kuwa sehemu bora katika ujenzi na ukomavu wa Fikra chanya kwa maisha ya Mtanzania wa leo, Na kuifanya Tanzania yote kupitia vijiji vyote kuwa pamoja na kufikri pamoja na kuungana pamoja kuisadia Tanzania katika nyanja zote za kijamii, kisiasa, kimazingira na kiuchumi. Kijijifamiliy ni familia ya pamoja ya Wanakijiji katika ushiriki katika hatua zote za utekelezaji wa wajibu chanya kwa misingi shirikishi na ambatano, kwa misingi ya kuzifanya familia za watanzania kufahamu wajibu wao katika kuhakikisha maendeleo yanapatikana na kuhimiza,kukuza maadili katika jamii kwa ujumla .

KIJIJIfamily ni Maisha halisia katika maisha ya wanakijiji ya kila siku na kinapiga hatua kadiri wanakijiji wanavyopiga hatua katika kutekeleza wajibu na kutimiza malengo yao. Kijiji na ni rafiki kwa wote kwa maslahi ya Umma na faida ya Taifa! Kijiji ni rafiki wa Vijiji vyote na mitaa yote, inayohitaji mabadiliko katika wajibu, fursa na haki.

KIJIJIfamily kitawakutanisha wanachama wote na kuweka uhalisia wa pamoja wa kufahamiana kwa namba za simu na sehemu zao wanazoishi. Wanachama watajadili mada facebook katika mijadala chanya na kufikiria kuanza mijadala ya wazi katika sehemu itayopendekezwa na baadaye kurushwa kwenye vituo vyetu vya Runinga kwa lengo la kuhakikisha watanzania wanapata zao chanya na pia kijiji kuazisha family monthly parties ili wanakijiji waweze badilishana mawazo na kujenga familia katika kuendeleza kusudio chanya na HAI.

Pamoja Daima na Kijiji Kidumu katika Kusaidia Gurudumu la Uchumi wa Taifa Letu.