Kijiji cha kibao

Kijiji cha Kibao ni moja ya vijiji katika kata ya Mtwango tarafa ya Ifwagi, wilayani Mufindi. Hapa palikuwa makao makuu ya wilaya kabla ya kuhamishwa miaka ya 80's. Chimbuko la jina hili (KIBAO) ni kibao kilichokuwa maeneo ya pale Polisi (njia ya kwenda Luiga penye mnara wa Uhuru) kikionesha zilipokuwa ofisi za mabasi ya "Relwe". Watu wanaposafiri walikuwa wakisema "nashukia Kibaoni" ndipo ikawa chimbuko la jina KIBAO. Uwepo wa mitandao ya kijamii unatupa nafasi wazaliwa, waalikwa na wote wanaoifahamu Kibao kubadilishana mawazo yenye mbegu za mapinduzi ya kimaendeleo mahali popote tuliko. Twende pamoja!