Kwaya za A.I.C.

Kundi hili ni la Kikristo na Wakristo tu, Maalum kwa WADAU wa Kwaya za A.I.C.
Kufundishana, Kupashana habari, kuonyana, kujadili na Kujengana kuhusu uimbaji wa Kwaya za A.I.C.

VIGEZO NA MASHARTI:-

1. MAUDHUI:
Hoja zote sharti ziwe za mlengo wa Kwaya za A.I.C. Hoja, picha ama video yoyote isiyoendana na Maudhui ya jina la Kundi itaondolewa mara moja.

2. UMAKINI:
Unapoweka hoja, Neno YESU, MUNGU, BWANA, ROHO MTAKATIFU na JEHOVA lazima yaandikwe kwa Umakini wake ukizingatia uandikaji wake kwa herufi KUBWA Mwanzo wa neno. Usipozingatia hilo, hoja yako itaondolewa.

3. UHURU:
Kila mwanachama ana haki ya kuweka ama kuchangia hoja kwa uhuru. Na kila mchangiaji anatakiwa kuheshimu mawazo ya kila mtu.

4. LUGHA:
Mada lazima iwe katika LUGHA ya KISWAHILI, ila katika kuchangia hoja mchangiaji unaruhusiwa kutumia Lugha yoyote unayoimudu.

5. USTAWI WA KUNDI:
Hoja yoyote itakayopelekea wachangiaji kulumbana kwa maneno makali ya dharau, kejeli, kebehi ama vijembe; Admin, Mtoa hoja, au mtu yeyote atatoa dira ya mwelekeo wa mjadala. Kama ushauri huo utapuuziwa na wachangiaji, Post
hiyo itaondolewa mara moja kulinda heshima na hadhi ya kundi.

6. MAKWAZO:
(a). Ni marufuku kupandikiza chuki dhidi ya Kundi hili.
(b). Ni marufuku kuweka mijadala ya kujadili maisha binafsi ya mwanachama ama mchangiaji ama watu wengne watakaoguswa na mjadala husika.
(c). Ni marufuku Kubaguana katika mijadala kwa misingi ya Elimu na Ukanda.
(d). Ni marufuku Kutumia maneno ya Matusi, kebehi, vijembe, kejeli, dharau ama maneno ya kudharirisha utu wa mtu ama ya kufanana na hayo yakimlenga mtu binafsi ama kundi kwa ujumla wake.
Atakayekiuka, hoja yake itaondolewa mara moja. Pia yeye atafutwa katika kundi mpaka atakapoomba tena kujiunga baada ya miezi mitatu (3) kupita. Ushahidi utatokana na malalamiko ya wahusika.

7. PROMOSHENI:

Tangaza au Promote Kwaya yoyote kwa kazi zao na huduma yao. Mfano Matoleo ya Kwaya, Uzinduzi na Album Mpya, Huduma watakayokuwa nayo katikati ya Juma ama Mwisho wa wiki na Mahali watakapokuwa.

MARUFUKU
(a) Kutumia KUNDI hili kutangaza blogs au websites za kwaya, kikundi au mtu.
(b) Kutumia kundi hili Kupromote groups na Kurasa/pages zilizoko facebook. .
(c) Kuweka taarifa ya kwaya ikiwa haijakamilika kisha kuelekeza kuwa taarifa hiyo inapatikana mahali kwingine nje ya Kundi hili kupata taarifa kamili.
(d) Kuweka Matangazo yoyote ya kibiashara bila idhini.

Atakayekiuka, post yake itaondolewa mara moja. Ikijirudia, mhusika ataondolewa ndani ya Group.

Marufuku hii haitazingatia Maudhui ya hizo groups, Kurasa, blogs au websites.

KARIBU SANA

Contacts us:

+255 717 201 326.

[email protected]